SIMBA SC imepata ushindi kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup hatua ya fainali ikipata ushindi mbele ya mpinzani wake mkubwa Azam FC.
Bao la ushindi limefungwa na Yahya Zayd kiungo wa Azam FC ambaye alijifunga dakika ya 62 wakati akipambana kuokoa faulo iliyopigwa na kiungo Ellie Mpanzu.
Hili linakuwa taji la nne kwa Simba SC ikirejea bara na ushindi ikitwaa taji ambalo lilikuwa mikononi mwa Yanga SC waliofungashiwa virago na Azam FC.
Msimu wa 2025/26, Simba SC vs Azam FC zimekutana mara 3 ambapo kila timu imepata ushindi mara moja, Azam FC ilipata ushindi wa mabao 2-0 katika ligi na Simba SC imepata ushindi kwenye mchezo wa fainali.
Mchezo mmoja wa mzunguko wa pili kwenye ligi walitoshana nguvu wakigawana pointi mojamoja ndani ya dakika 90.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya ipo tayari jikoni inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata itakuwa mezani kuanzia Julai 10,2026.