Msichana wa Maisha Yangu mezani Julai 10, 2026

Tatizo la ajira lilikuwa limeota sugu katika kichwa cha Steven ambaye awali kabla ya kufika Dar aliamini kila mtu mjini ana kazi nzuri na ana hela zakutosha. Alizunguka kila ofisi na bahasha yake ya khaki iliyokuwa na CV milango ilikuwa migumu mithili ya chuma cha pua.

Aliitambua kuna siri nzito nzito kuhusu wadukuaji wa akaunti, mbinu wanazotumia, namna ya kujilinda na tatizo la udukuzi katika mitandao. Sio serikalini wala kampuni binafsi mfumo mkubwa ulikuwa unatumika hapo ndipo patashika na nguo kuchanika…

Kwa Steven kukosa anachokitafuta kulimfanya akumbwe na jambo jingine baya zaidi ambalo ni tatizo ya afya ya akili, mawazo yalimzidi uwezo hali hiyo ilipelekea apate ajali mbaya ya gari alipokuwa akivuka barabara ya Shekilango kituo cha Mapambano…

Ni nini hatma ya maisha yake na ujuzi alionao? Tatizo la ajira alilikabili namna gani? Majibu yote yapo katika kitabu cha Msichana wa Maisha Yangu.

Kutoka kwa Best Seller Author… Lunyamadzo Mlyuka, A Boy From Njombe tunaomba oda kupitia 0756 028 371