Hiki hapa kikosi cha Simba SC vs Azam FC, fainali CRDB

Kikosi cha Simba SC dhidi ya Azam FC katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB tayari kimetangazwa.

Ni Mzizima Dabi ambao utakwenda kumpata bingwa mpya mara baada ya mabingwa watetezi Yanga SC kuishia hatua ya nusu fainali.

Azam FC waliwaondoa Yanga SC kwa ushindi wa mabao 3-2 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa. Leo atakwenda kujulikana bingwa.

Kikosi cha Simba SC Kama langoni atakuwa Djibrilla Kassali akisaidiwa na Duchu, Kibabage, Rushine na Ismael Toure.

Wengine wanaoanza kwenye mechi hii itayoanza saa 11 jioni hii ni; Yusuph Kagoma, Libase Gueye, Neo Maema, Elie Mpanzu, Clatous Chama na Anicet Oura hawa watakuwa kikosi cha kwanza.

Wachezaji wa akiba ni Abel, Alexander, Kapombe, Mligo, Vedastus, Semfuko, Morice, Kante, Seleman Mwalimu na Inno.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.