Yanga SC 3-0 TRA United, NBC Premier League

Yanga SC 3-0 TRA United ni matokeo ya mchezo uliochezwa leo Juni 27,2026 Uwanja wa KMC Complex ikiwa ni mzunguko wa pili.

Mabao yote yamefungwa na kiungo mshambuliaji Allan Okello ambaye amefunga hattrick ilikuwa ni dakika ya 38, 51 kwa mkwaju wa penati na kamba ya tatu ilifungwa dakika ya 60.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wababe hawa waligawana pointi mojamoja kwa sare ya bila kufungana huku Juni 27, 2026 mabingwa watetezi wakishusha kichapo dhidi ya TRA United.

Yanga wanafikisha alama 72 na mchezo wao wa mwisho watacheza na JKT Tanzania na wakishinda watakuwa mabingwa bila hata kujali matokeo ya Simba SC katika mchezo huo kwa kuwa tofauti yao ni pointi 2 mpaka sasa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.