Canada Yaanza Kombe la Dunia kwa Sare ya Kusisimua dhidi ya Bosnia

Mshambuliaji wa Canada, Cyle Larin, alitokea benchi na kuisadia timu yake kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Bosnia na Herzegovina katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi B wa Kombe la Dunia uliochezwa Ijumaa mjini Toronto.

Bosnia ilianza vizuri baada ya Jovo Lukic kufunga bao la kuongoza dakika ya 21 kwa kichwa, likiwa bao lake la kwanza katika timu ya taifa.

Canada iliongeza kasi ya mashambulizi kipindi cha pili na ilikaribia kusawazisha kupitia Richie Laryea, lakini beki Sead Kolasinac aliokoa bao kwa ustadi mkubwa baada ya kuondoa mpira uliokuwa unaelekea wavuni.

Licha ya kutawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi, Canada ilishindwa kutumia vyema nafasi zake hadi dakika ya 78, pale Larin alipoingia akitokea benchi na kufunga bao la kusawazisha dakika chache tu baada ya kuingia uwanjani, akiwapa furaha mashabiki wa nyumbani.

Bao hilo limeingia kwenye historia kama bao la kwanza la Canada kufungwa katika Kombe la Dunia lililoandaliwa nyumbani, huku likiiwezesha timu hiyo kupata pointi yake ya kwanza kabisa katika historia ya mashindano hayo.

Nyota mwingine wa Canada, Jonathan David, alipata nafasi nzuri mapema mchezo lakini shuti lake liliokolewa na kipa Nikola Vasilj.

Kwa upande wa Bosnia, Ermedin Demirovic naye alikaribia kuongeza bao la pili lakini kipa wa Canada, Maxime Crepeau, aliokoa hatari hiyo kwa ustadi mkubwa.

Matokeo hayo yanaipa Canada mwanzo wa matumaini katika mashindano hayo, ingawa walitamani kuanza kwa ushindi mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.