Simba SC 4-0 TRA United CRDB Federation Cup ni matokeo rasmi kwenye mchezo wa leo Mei 17, 2026 Uwanja wa KMC Complex hatua ya robo fainali.
Matokeo haya yanaipa tiketi Simba SC kutinga hatua ya nusu fainali ambapo itakutana na Coastal Union iliyopata ushindi mbele ya Singida Black Stars kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Katika mchezo wa leo magoli ya Simba SC yalifungwa na Clatous Chama dakika ya 6, Anicent Oura dakika ya 26, Seleman Mwalimu dakika ya 64 na Bashiri dakika ya 78.
Nyota Chama ndani ya Mei amekuwa kwenye ubora kutokana na mwendelezo kwenye mechi za ushindani anazopata nafasi ya kucheza chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker.
Katika mechi 4 za ligi amefunga magoli 5 na kutwaa tuzo ya Man of the Match kwenye mecho zote nne mfululizo na leo amefunga goli la ufunguzi dhidi ya TRA United hatua ya robo fainali.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.