Mashujaa FC 0-1 Azam FC, CRDB Federation Cup ni matokeo rasmi kwenye mchezo wa leo Mei 17, 2026 hatua ya robo fainali CRDB Federation Cup.
Matajiri wa Dar wameibuka na ushindi huo katika Uwanja wa Lake Tanganyika mwisho wa reli Kigoma kwa goli ambalo lilipachikwa dakika 45 za mwanzo.
Anaitwa Idd Suleman maarufu kwa jina la Nado alipachika goli hilo dakika ya 45+4 likadumu mpaka mwisho wa mchezo.
Wababe hao wanasonga mbele hatua ya nusu fainali wanakwenda kukutana na mabingwa watetezi Yanga SC ambao waliifungashia virago JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa Mei 16, 2026.
Wawili hawa kila mmoja alikuwa ugenini kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali, Yanga SC Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo na Azam FC, Kigoma.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.