Coastal Union yaitisha Singida Black Stars

Coastal Union yatisha Singida Black Stars kuelekea kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali CRDB Federation Cup leo Mei 16, 2026.

Ni Coastal Union vs Siginda Black Stars mchezo mkali unaotarajiwa kuchezwa saa 10 jioni kwa wababe hawa kusaka tiketi kutinga hatua ya nusu fainali.

Mabingwa watetezi wa taji hili ni Yanga SC ambao watashuka uwanjani kusaka ushindi dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo.Wababe hawa wawili wanatarajiwa kumenyana leo Mei 16, 2026 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kusaka tiketi ya kutinga nusu fainali.

Hussen Mchovu, Ofisa Habari wa Coastal amesema: “Tunataka kuwashona kwa mara nyingine Singida, tuliwafunga magoli mawili mchezo wa ligi tukiwa pungufu kwa kuwa mlinda mlango wetu alionyeshwa kadi nyekundu leo tunaanza tukiwa kamili hivyo tutapambana,”.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo ndani ya kikosi cha Coastal Union ni Shiza Kichuya, Abdalah Denis, Saad Mwanza.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.