Yanga SC vs Azam FC Nusu fainali Muungano Cup ya kwanza Zanzbar kwa wababe hawa wawili kukutana ndani ya dakika 90 kusaka tiketi ya kutinga hatua ya fainal.
Ipo wazi kwamba mabingwa watetezi wa taji hili ni Yanga SC iliyoanza kutinga hatua ya robo fainali kwa kupataushindi kwenye mchezo wa ufunguzi, hatua ya robo fainali.
Wababe hawa wanatarajiwa kukutana 25/4/2026, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar katika mchezo mkali wa Nusu Fainali ya kwanza, ya mashindano ya Muungano Cup 2026.
Inakuwa ni Dar es Salaam Derby ndani ya Zanzibar kwenye Muungano Cup.
Yanga SC imefika hatua hiyo baada ya kuifunga Muembe Makumbi City 4-0 katika Robo Fainali, Azam FC imepata ushindi mbele ya KVZ FC 2-0 Jean-Jacque Ngitta ni mfungaji pekee wa magoli kwenye mchezo wa robo fainali.
Kwa Yanga SC ni Prince Dube na Shekhan hawa walifunga magoli mawilimawili kila mmoja.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.