Simba SC leo inashuka Uwanja wa New Amaan kusaka ushindi mbele ya Mafunzo FC hatua ya robo fainali Muungano Cup.
Ni wazi kuwa Mafunzo FC wanahitaji ushindi kwenye mchezo wa leo hivo ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa kwa timu zote mbili.
Katika kikosi cha Simba SC ni Hussen Abel ameanza langoni wachezaji wengine ni Duchu, Mligo, Vedastus, Mbegu, Semfuko, Ladack Chasambi, Inno Loemba, Baraka, Abraham Morice na Bashiri wameanza kikosi cha kwanza.
Kiungo Bajaber ameanza benchi akiwa na Alexander, Kapombe, De Reuck, Yusuph Kagoma, Kante, Seleman Mwalimu, Clatous Chama na Gueye.
Mshindi wa mchezo wa leo hatua ya nusu fainali atamenyana na Mlandege iliyowafungashia virago Singida Black Stars.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.