Wakali za pasi za magoli NBC Premier League

Katika nyota 7 wa NBC Premier League wenye pasi nyingi 2025/26 kinara katika eneo hili ni kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum mwenye pasi 7 za magoli.

Azam FC imekuwa kwenye mwendo bora ndani ya uwanja ikiwa ni timu namba moja kukusanya sare nyingi ambazo ni 10 na haijapoteza kwenye mechi 19 sawa na Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Pedro Gonalves.

Kwenye orodha ya wakali wa kutengeneza pasi za mwisho, Simba SC ina jina moja la Ellie Mpanzu ambaye ametoa jumla ya pasi 5 za magoli.

Mpanzu ni miongoni mwa wachezaji wa Simba SC anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokabiliana na Namungo FC, kesho Aprili 19, 2026 Uwanja wa Majaliwa mchezo wa NBC Premier League.

Yanga SC ina orodha ya wachezaji wanne ambao ni Allan Okello mwenye pasi 6 za magoli, Duke Abuya mwenye pasi 5.

Israel Mwenda na Maxi Nzengeli hawa wawili kila mmoja ametengeneza jumla ya pasi 4 za magoli sawa na Ibrahim Imoro wa Singida Black Stars.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.