Simba SC yawafuata Namungo FC kamili gado

KIKOSI cha Simba SC kimewafuata wapinzani wao Namungo FC kamili gado kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Aprili 19, 2026 Uwanja wa Majaliwa.

Chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker kikosi hicho kimewasili Ruangwa, Lindi mara baada ya kuanza safari kikitokea Dar.

Ikumbukwe kwamba kikosi cha Simba SC kimetoka Arusha ambapo kilikuwa na mchezo wa NBC Premier League vs Fountain Gate.

Kwenye mchezo uliopita kilipata ushindi wa magoli 3-0 huku mchezaji bora wa mchezo akiwa ni kiungo Clatous Chama.

Wababe hawa wanatarajiwa kukutana saa 1:00 usiku kwenye msako wa pointi 3 muhimu ndani ya dakika 90.

Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya mechi 18 ikiwa na pointi 39 Namungo FC ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 22 zote zimecheza mechi 18.

Miongoni mwa wachezaji wa Simba SC waliopo kwenye msafara ni Duchu, De Reuck, Shomari Kapombe, Ellie Mpanzu.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.