Kocha Stars abainisha sababu yakupoteza

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa kushindwa kutumia nafasi mbili ambazo walipata kwenye mchezo ni sababu kushindwa kupata ushindi.

Tanzania 0-1 Liechtenstein ni matokeo kwenye mchezo uliochezwa Machi 26,2026 kwenye FIFA Series, Uwanja wa Kigali, Rwanda.

Gamondi amesema: “Kila mwenye macho ameona, tulipata nafasi mbili tukashindwa kuzitumia na tumepoteza mchezo hakuna kingine ambacho ninaweza kusema zaidi ya kuwaomba msamaha Watanzania. Mpira ni kufunga.

“Wapinzani wetu walitumia nafasi ambayo wameipata na kufanya matokeo kuwa namna hiyo, hakuna ambaye alikuwa anapenda kuona tunapoteza mchezo lakini haya ni matokeo,”.

Tanzania ilipoteza kwenye mchezo huo wa kirafiki kipindi cha pili baada ya dakika 45 za mwanzo ubao kusoma 0-0.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.