Yanga Yatinga nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026

YANGA wametinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya TRA United, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Bao hilo lilipatikana dakika ya 31 kupitia Ecua na kuipa Yanga tiketi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Katika hatua ya nusu fainali, Yanga SC itamenyana na Singida Black Stars, huku Simba SC wao wakivaana na Azam FC (Wanalambalamba) kusaka nafasi ya kucheza fainali.

FT: Yanga SC 1–0 TRA United
⚽ 31’ — Ecua