Beki wa Manchester City, Rúben Dias, atakaa nje ya uwanja kwa takribani wiki 6 baada ya kupata majeraha ya msuli wa paja (hamstring).
Jeraha hilo ni pigo kubwa kwa kikosi cha City katika kipindi hiki cha ushindani mkali, huku kocha Pep Guardiola akilazimika kupanga upya safu ya ulinzi.
Taarifa zinasema Dias ataanza mara moja programu ya matibabu na uangalizi maalum ili kurejea uwanjani akiwa salama bila hatari ya kurudia jeraha.
Man City Yabaki na Wasiwasi Baada ya Dias Kuumia