Shirikisho la soka la Nigeria limekanusha ripoti zinazodai kuwa Wachezaji wawili Victor Osimhen na Akor Adams kuwa wameondoka kwenye kambi ya Super Eagles nchini Morocco katika Mashindano ya AFCON.
Shirikisho pia limetupilia mbali madai ya kuwepo kwa mpasuko kati ya Osimhen na Ademola Lookman.
Limeeleza kuwa masuala yaliyotokana na mabishano ya Uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Msumbiji yalikuwa yametatuliwa ndani.
Nigeria iliichapa Msumbiji 4-0 na kujihakikishia kufuzu kwenye robo fainali ya AFCON siku ya Jumatatu.