TIMU ya taifa ya Misri inakuwa ya kwanza kutinga katika hatua ya mtoano baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 Afrika Kusini. Kwenye mchezo wa hatua ya makundi uliochezwa nchini Morocco kwa kundi B pointi tatu zimebebwa na Misri. Goli pekee la Mohamed Salah kwa mkwaju wa penalti dakika ya 45 limeipa ushindi Misri.
Misri kwenye mchezo wa leo walikuwa pungufu. Mchezaji Mohamed Hany alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano. Licha ya kadi hiyo dakika ya 45+2 bado goli la Salah lilidumu mpaka mwisho wa mchezo wakitinga hatua ya 16 bora.
Kadi za njano
Dakika ya 20 Teboho Mokoena alionyeshwa kadi ya njano kwa Afrika Kusini.
Dakika ya 30 Mohamed Hany alionyeshwa kadi ya njano kwa Miari.
Dakika ya 43 Lyle Foster alionyeshwa kadi ya njano kwa Afrika Kusini
Dakika ya 43 Khuluso Mudau alionyeshwa kadi ya njano mwa Afrika Kusini.
Misri katika kundi B mchezo wa ufunguzi ilipata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Zimbabwe. Licha ya mchezo wa kwanza kutengeneza nafasi nyingi na kumiliki mpira kwa asilimia kubwa walifungwa goli mapema. Dakika ya 20 ni Prince Dube alifunga goli kwenye mchezo huo.
Misri waliweka usawa kupitia magoli ya Omar Marmoush dakika ya 64. Mohamed Salah alifunga goli la ushindi. Hivyo Misri walifanya Comeback kwenye mchezo wa ufunguzi wakivuna pointi tatu mazima.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.