SIMBA YAFUNGUKIA UGUMU WA BRAVOS

SIMBA inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids imeweka wazi kuwa inakwenda kukutana na mpinzani mgumu ndani ya dakika 90 kutokana na mwendo wake wa kupata matokeo mazuri kwenye mechi za nyumbani ndani ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Wakiwa na kumbukumbu ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo waliocheza nao Bravos, Uwanja wa Mkapa Novemba 24 2024 ubao uliposoma Simba 1-0 Bravos, watakabiliana nao kwa mara nyingine, wakiwa ugenini.

Tayari kikosi cha Simba kimewasili Angola kwa  maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Januari 12 2025 kwa wababe hao kutoka kundi A kusaka pointi tatu muhimu katika kusaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali huku kocha akisema kuwa ni mchezo mgumu kwao.

“Tunakwenda kucheza mchezo mgumu hasa ukizingatia kwamba wapinzani wetu Bravos wamekuwa na mwendo mzuri kwenye mechi ambazo wanacheza wakiwa nyumbani hivyo tunakwenda kwa tahadhari na malengo ni kuona kwamba tunapata ushindi.

“Wachezaji wamekuwa wakijituma hilo tunajivunia na wanastahili pongezi licha ya ugumu ambao upo kwenye mechi zetu wamekuwa wakifanya vizuri na tunapata matokeo, bado tuna kazi kubwa ambayo tunakwenda kuifanya, kikubwa ni utayari na tunaamini kwamba tutapambana ili kupata kile tunachokifuta.”

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.