KOCHA Msaidizi wa Yanga, Abdihamid Moalin amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Al Hilal utakuwa ni mgumu lakini wapo tayari kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu kutokana na umuhimu wa mchezo huo kwa Yanga.
Ikiwa Yanga itapata pointi tatu kwenye mchezo huo itabakiwa na mchezo mmoja Uwanja wa Mkapa ambao huo utaamua hatima ya timu hiyo kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mchezo huo Yanga inatambua kwamba wapinzani wao wanatumia nguvu nyingi kwenye mipira ya kushtukiza huku ulinzi wao ukiwa imara kwa kuwa nit imu yenye safu imara ya ulinzi.
Kocha huyo amebainisha kwamba wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo na wanakwenda wakiwa na ari ya kusaka ushindi ndani ya dakika 90 hivyo wataingia kwa tahadhari kusaka ushindi kwenye mchezo huo mgumu.
“Tunakwenda tukiwa na Imani kwamba tutapata pointi tatu muhimu, tunatambua kwamba hautakuwa mchezo mwepesi lakini tupo tayari na wachezaji wanajua kwamba huu ni mchezo muhimu kwetu kutafuta pointi tatu muhimu.
“Kikubwa ni utayari na mchezo wetu upo wazi kwamba walipata ushindi kwenye mchezo wetu uliopita, tunahitaji kufanya vizuri katika mchezo wetu na tupo tayari mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi na tutapambana kupata matokeo mazuri.”
Tayari kikosi cha Yanga kimewasili Mauritania kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Januari 12 2025.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.