Derby ya London Yapamba Moto leo: Palace Wawakaribisha West Ham Selhurst Park

Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)

 

Uwanja wa Selhurst Park, London Leo tarehe 20 kuanzia saa 22:00 utakuwa jukwaa la pambano la kusisimua la derby ya London kati ya Crystal Palace dhidi ya West Ham United katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Mchezo huu unakuja wakati timu zote zikiwa na malengo tofauti kwenye msimamo, huku Crystal Palace wakiwa na rekodi nzuri ya nyumbani katika derby hizi baada ya kushinda mechi 3 kati ya 5 za mwisho za Selhurst Park dhidi ya West Ham.

Ushindi wa Palace wa mabao 2-1 kwenye uwanja wa London Stadium mnamo Septemba 20, 2025, ulioweka Presha kwa kocha wa West Ham wakati huo, Graham Potter, na unaonyesha kuwa Eagles wamekuwa wakiibuka na ubabe katika derby za hivi karibuni

Katika michezo 5 ya mwisho kati ya timu hizi, Palace wameibuka na ushindi mara 2 (wakiwemo ushindi wa 2-1 Septemba 20, 2025 na 2-0 Januari 18, 2025), West Ham ushindi mara 1 (2-0 Agosti 24, 2024), na sare mara 2.

Mechi ya mwisho kati ya timu hizi ilipigwa Septemba 20, 2025 kwenye uwanja wa London Stadium na kumalizika kwa ushindi wa Crystal Palace wa mabao 2-1, ambapo Jean-Philippe Mateta na Tyrick Mitchell walifunga mabao ya Palace huku Jarrod Bowen akifunga la West Ham.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa upande wa majeraha Crystal Palace watawakosa nyota wao muhimu Nketiah Eddie na Evann Guessand, jambo linalopunguza ubunifu wa safu ya mashambulizi ya Palace. Hata hivyo, Jean-Philippe Mateta ambaye amekuwa akifunga mara kwa mara katika mechi za nyumbani, anatarajiwa kuwa tishio kubwa kwa ulinzi wa West Ham.

Kwa upande wa West Ham,wana matumaini na Jarrod Bowen ambaye alifunga bao lao pekee katika mechi ya Septemba 20, 2025, huku Tomás Souček akitarajiwa kuwa nguzo kwenye safu ya kiungo kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao ya kichwa kutoka kwenye vipa pembe. Jisajili