LEO Aprili 26, 2026 mchezo wa Hatua ya Nusu Fainali ya Muungano Cup 2026 utapigwa kwa wababe wawili kusaka tiketi kusonga hatua ya fainali.
Ni katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, Simba SC vs Mlandege FC, nusu Fainali ya pili ya mashindano haya.
Mshindi wa mechi hii atavaana naYanga SC iliyopata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa fainali ya kwanza Aprili 25, 2026.
Mara ya mwisho timu hizi zilipokutana ubao wa matokeo ulisoma Mlandege FC 1-0 Simba SC 13/1/2024 katika mchezo wa Fainali ya Mapinduzi Cup.
Beki wa Simba SC, Duchu amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo hivyo watapambana kupata ushindi ndani ya dakika 90.
“Tunatambua mchezo utakuwa mgumu, tupo tayari kwa ushindani kutokana na maandalizi ambayo tumefanya hivyo mashabiki wajitokeze kuwa pamoja nasi,”.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.