YANGA KAZINI TENA LEO AMAAN

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Yanga leo wanakazi ya kusaka ushindi mbele ya KMKM mchezo unaotarajiwa kuchezwa saa 10:15 jioni.

Ni Uwanja wa Amaan mchezo huo unatarajiwa kuchezwa mbele ya mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kushuhudia burudani.

Mchezo wa kwanza wa Yanga ilikuwa mbele ya Taifa Jang’ombe na iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ambapo nyota Dennis Nkane na Heritier Makambo waliweza kutupia.

Pia nyota wapya ambao wamesajiliwa na Yanga ikiwa ni pamoja na Salum Aboubakhari, ‘SureBoy’, Crispin Ngushi na Nkane waliweza kupata nafasi ya kuonyesha makeke yao huku langoni akiwa kijana Aboutwalib Mshery.

Kwa mujibu wa Hassan Bumbuli, Mkuu wa kitengo cha Habari amesema kuwa wapo tayari na wanahitaji taji hilo.