BAADA ya Keneth Muguna wa Azam FC kufunga mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi na kupewa zawadi ya laki tano na NIC Tanzania, kazi yao inayofuata ni dhidi ya Yosso Boys,Januari 8.
Alipewa zawadi hiyo baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Amaan.
Ilikuwa ni dakika 66 alipachika bao hilo baada ya piga nikupige kwenye lango la Namungo.
Leo kazi inaendelea ambapo inatarajiwa kuwa namna hii:-
Yanga v KMK saa 10:15
Simba v Mlandege FC,saa 2:15