Home Sports SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MLANDEGE

SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MLANDEGE

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mlandege.

Leo saa 2:15 usiku Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Mlandege mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Amaan.

Pablo amesema kuwa wachezaji wanajua majukumu yao na wapo tayari kwa ajili ya mchezo ili wapate pointi tatu.

“Tunajua kwamba mchezo wetu muhimu na tunahitaji matokeo, kikubwa ni pointi tatu ambazo zitatufanya tuweze kutoka hapa tulipo.

‘Jambo ambalo nina uhakika nalo ni kwamba wachezaji watacheza na kupambana kwa ajili ya ushindi, wapinzani wetu tunawaheshimu lakini tunatakiwa kufuzu hatua inayofuata,”.

Mchezo wa Simba wa ufunguzi katika Kombe la Mapinduzi ilikuwa dhidi ya Selem View na ilishinda kwa mabao 2-0.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA
Next articleYANGA KAZINI TENA LEO AMAAN