KIUNGO mshambuliaji ndani ya kikosi cha Azam FC, Feisal Salum gari limewaka huko kutokana na kasi yake ya kucheka na nyavu kuendelea kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.
Wakati ubao wa Uwanja wa Azam Complex, Novemba 28 2024 ukisoma Azam FC 2-1 Singida Black Stars ambayo imetoka kuachana na Patrick Aussems ambaye alikuwa kocha mkuu alipachika bao moja kwenye mchezo huo.
Ni dakika ya 38 alipachika bao hilo kipindi cha kwanza na bao la pili la ushindi kwa Azam FC lilipachikwa na Jhonier Blanco dakika ya 57. Bao pekee kwa Singida Black Stars lilipachikwa na Elvis Rupia dakika ya 62.
Ushindi huo unaifanya Azam FC kuwa nafasi ya pili kwenye msimamo pointi 27 baada ya kucheza mechi 12 na vinara ni Simba wenye pointi 28 tofauti ya pointi moja huku Simba ikiwa imecheza mechi 11.
Feisal anafikisha mabao matatu ndani ya ligi msimu wa 2024/25 ambapo mabao yote matatu amefunga katika Uwanja wa Azam Complex.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.