AJIBU APIGA HESABU NDEFU

BAADA ya kusaini dili la mwaka mmoja ndani ya kikosi cha Azam FC kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu amepiga hesabu ndefu za kufanya vizuri kwa ajili ya Tanzania na mashabiki wa Azam FC.

Desemba 30 Ajibu ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Simba alitambulishwa rasmi Azam FC kwa kandarasi ya mwaka mmoja.

Anakuwa ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya kikosi hicho akipewa mikoba ya Salum Aboubhakar, ‘Sure Boy’ ambaye ameibukia ndani ya Yanga.

Kiungo huyo amesema:”Nafurahi kupata nafasi ndani ya Azam FC imani yangu ni kwamba nitafanya vizuri kwa ajili ya Tanzania na mashabiki wa Azam FC.

“Azam FC ni moja ya timu kubwa na nitakapoanza mazoezi nitaonyesha kile ambacho ninahitaji kufanya imani yangu kila kitu kitakwenda vizuri,” amesema.

Ajibu amekabidhiwa pia jezi namba 8 ambayo ilikuwa inavaliwa na Sure Boy.