NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hawakutumia nafasi ambazo walizitengeneza kwenye mchezo wao dhidi ya Simba.
Desemba 11, Uwanja wa Mkapa ulikamilika kwa timu mbili za Simba na Yanga kutoshana nguvu bila kufungana.
Nabi ameweka wazi kwamba hakukuwa na timu ambayo ilikuwa na uhakika wa kupata ushindi kwenye mchezo huo kwa kuwa ilikuwa ni salimia 50/50 kwa kila timu.
“Awali niliweka wazi kwamba mchezo wetu wa dabi ni nusunusu kwa kila timu kupata ushindi na imetokea hivyo hakuna wa kumlaumu kwa kuwa ni mpira.
“Naweza kusema kwamba hatukutumia nafasi ambazo tulizitengeneza kwenye mchezo wetu na hilo limetufanya tushindwe kupata ushindi lakini wachezaji walicheza vizuri,” amesema.
Yanga inafikisha pointi 20 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 18 baada ya kucheza mechi nane.