YANGA:MOTO HAUZIMI

NYOTA wa Yanga, Said Ntibanzokiza ameweka wazi kuwa moto wake ambao ameuwasha ndani ya ligi hautazima kwa kuwa anamalengo makubwa katika kutimiza majukumu yake.

Kwenye mabao 12 ambayo yamefungwa na timu hiyo ametupia mabao mawili na yote ni kwa mapigo huru ilikuwa mbele ya Namungo alipofunga kwa penalti na mbele ya Mbeya Kwanza alipofunga kwa pigo la faulo.

Ntibanzokiza amesema kuwa kasi ambayo ameanza nayo itaendelea bila kupoa kwa kuwa kazi yake yeye ni mpira.

“Kazi yangu ni mpira na uwezo wangu upo wazi hasa ukizingatia kwamba nipo na wachezaji ambao wananipa ushirikiano mkubwa hivyo sina mashaka kuhusu kile ambacho ninakifanya na nina amini kwamba nitaendelea kuwa imara.

“Kila mchezo kwetu ni muhimu na ambacho tunahitaji ni kuona kwamba tunapata pointi tatu, mashabiki wazidi kuwa bega kwa bega nasi tunaamini kwamba hatutawaangusha,” amesema.

Desemba 11 kikosi cha Yanga kitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Simba baada ya kutoka kusepa na pointi tatu mbele ya Mbeya Kwanza.