Simba SC yatupia mabao 19 NBC Premier League

Katika Ligi Kuu ya NBC safu ya ushambuliaji ya Simba SC 2026/27 baada ya mechi 8 inaongoza kwa kuwa na kasi katika kucheka na mabao ikifunga 19.

Mchezo pekee iliyovunja rekodi kwa kufunga mabao mengi ilikuwa Simba SC 6-1 Mashujaa FC uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar.

Baada ya ushindi huo ulifanya timu hiyo kufikisha jumla ya pointi 24 kibindoni ikiwa inaongoza ligi bado haijapoteza mchezo.

Simba SC inaongoza kufunga mabao mengi inafuatiwa na Yanga SC iliyo nafasi ya pili imetupia mabao 17 baada ya mechi 7. Singida Black Stars inafuata ikiwa na mabao 14.

Katika mabao hayo washambuliaji wawili Ismail Mgunda na Doumbia hawajafunga wala kutengeneza asisti katika mechi ambazo wamecheza.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema muda wa Doumbia kufunga upo karibu kutokana na uwezo alionao.

“Doumbia ni mshambuliaji mzuri na hakuna timu ambayo inasajili mchezaji ambaye hana uwezo. Muda wake wakufunga upo karibu na atawafurahisha Wanasimba,”.

…

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar

Moyo Wangu Unavuja Damu: https://selar.com/7901h4koj4