FT:CFFA 0-4 Yanga SC

Yanga SC imepata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CFFA katika mchezo wa mkondo wa Kwanza hatua ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ni Oktoba 16,2026 pambano hili kali limepigwa kwa wababe hawa kukutana uwanjani katika dakika 90 za kazi mwanzo mwisho.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Toure dakika ya 40, Albert Kangwanda dakika ya 47, Mudathir Yahya dakika ya 54 na Maxi Nzengeli dakika ya 59.

Yanga SC imeanza kwa ushindi mchezo wa kwanza wakiwa ugenini wanatanguliza mguu mmoja hatua ya makundi.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Oktoba 21 kwa wababe hawa wawili kusaka mshindi wa jumla atakayesonga mbele hatua inayofuata ya makundi.

…

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar

Moyo Wangu Unavuja Damu: https://selar.com/7901h4koj4