BAADA ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha umesoma Fountain Gate 1-1 Pamba Jiji FC, NBC Premier League.
Wababe hawa wawili wamegawana pointi mojamoja kwa kila timu kupata inachostahili katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Fountain Gate walipindua meza baada ya dakika 6 kupita muda waliofungwa bao la uongozi na wageni katika mchezo wa leo.
Ni Pamba Jiji FC walianza kucheka na nyavu mtupiaji Abdallah Ali dakika ya 6 kwa upande wa Fountain Gate ni Sadick Ramadhani dakika ya 12 aliweka msawa na kufanya mapumziko iwe ni 1-1.
Mpaka dakika 90 zinagota mwisho leo Oktoba 16,2026 hakuna nyavu za mlinda mlango ambazo zilitikishwa licha ya majaribio kadhaa kufanyika.
Timu zote zinasalia palepale zilipokuwa, Fountain Gate nafasi ya 16 na Pamba Jiji FC nafasi ya 15 zote zina pointi 5 kibindoni.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.
Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.
Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar
Moyo Wangu Unavuja Damu: https://selar.com/7901h4koj4