Kikosi cha Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi ni namba moja eneo la ufungaji. Safu hiyo ya ushambuliaji inayoongozwa na Peter Shalulile imeipoteza ile ya Simb SC inayoongozwa na Ibrahim Doumbia.
Yanga SC baada ya mechi 6 ambazo ni dakika 540, safu ya ushambuliaji imefunga mabao 16. Ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 16 msimu wa 2026/27.
Ni Singida Black Stars yenye Jonathan Sowah, hii ni namba mbili kwa safu kali za ushambuliaji ikiwa imetupia mabao 13 baada ya mechi 6 ikiwa na wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 41.
Simba SC ni namba tatu kwa timu zenye mabao mengi ikiwa imetupia mabao 11 ina wastani wakufunga bao 1 kila baada ya dakika 49. Timu hii inanolewa na Kocha Mkuu, Steve Barker imefunga mabao sawa na Azam FC iliyocheza mechi 7 ikiwa na wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 57.
Azam FC kwenye msimamo ni nafasi ya 3 imecheza mechi 7 ambazo ni dakika 630 imekusanya jumla ya pointi 14 huku Simba SC ikiwa na pointi 18 nafasi ya pili vinara ni Yanga SC wenye pointi 18.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.