Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Hispania, Luis de la Fuente, ameongeza mkataba mpya utakaomuweka kwenye nafasi hiyo hadi mwaka 2032.
Uamuzi huo unakuja baada ya De la Fuente kuiongoza Hispania katika kipindi cha mafanikio, akitwaa mataji matatu makubwa tangu alipoteuliwa kuwa kocha wa timu hiyo mwaka 2022.
Chini ya uongozi wake, Hispania ilishinda UEFA Nations League mwaka 2023, UEFA EURO 2024 pamoja na Kombe la Dunia la FIFA 2026, baada ya kuifunga Argentina katika fainali.
Mkataba huo mpya utamuwezesha De la Fuente kuendelea kuiongoza Hispania katika mashindano makubwa yajayo, yakiwemo EURO 2028, Kombe la Dunia 2030 na EURO 2032.
Katika kipindi chake cha uongozi, De la Fuente ameiweka Hispania katika kiwango cha juu kimataifa, huku akiwa ameshinda mechi 38 kati ya 50 alizoiongoza timu hiyo ya taifa.
Kwa kuongeza mkataba hadi mwaka 2032, De la Fuente ataendelea na jukumu la kuiongoza Hispania katika harakati za kuongeza mafanikio zaidi kwenye soka la kimataifa.