Union Berlin Kuikabili Schalke 04, Nani Kuibuka na Ushindi?

Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga itaendelea Ijumaa, Septemba 11, Union Berlin itakuwa mwenyeji wa Schalke 04 katika mchezo wa Bundesliga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Stadion An der Alten Försterei, Berlin. Mchezo huo utaanza saa 21:30 usiku, huku timu zote zikisaka ushindi wao wa kwanza msimu huu.

Union Berlin inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na pointi moja baada ya michezo miwili. Timu hiyo ilianza kwa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Eintracht Frankfurt kabla ya kukumbana na kipigo kizito cha 4-0 kutoka kwa Bayer Leverkusen katika mchezo uliopita. Matokeo hayo yameifanya Union kuwa na presha ya kupata ushindi mbele ya mashabiki wake.

Kwa upande wa Schalke, Chini ya kocha Miron Muslic timu hiyo imerejea Bundesliga baada ya kushinda taji la Bundesliga 2 msimu uliopita. Walianza kwa kufungwa 3-0 na Augsburg, lakini walionyesha uimara mkubwa katika mchezo uliopita kwa kupata sare ya 0-0 dhidi ya mabingwa Bayern Munich. Kipa Loris Karius alikuwa miongoni mwa nyota walioisaidia Schalke kupata pointi hiyo.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Schalke bado haijafunga bao katika ligi ya Bundesliga msimu huu, jambo linaloweka changamoto kubwa kwa safu yake ya ushambuliaji, kwani ni miongoni mwa timu tatu tu pekee katika Bundesliga ambazo bado hazijafunga bao lolote msimu huu.

Wakati huo huo, Union Berlin itahitaji kuboresha safu yake ya ulinzi baada ya kuruhusu mabao saba katika michezo yake miwili ya kwanza. Hivyo, uwezo wa kila upande kutumia nafasi utakuwa muhimu katika kuamua matokeo ya mchezo huu.

Kwa ujumla, mchezo huu unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa kwa sababu timu zote zinahitaji pointi tatu ili kuanza kujenga matumaini ya msimu mzuri. Union itatumia