MCHEZO wa NBC Premier League kwa wababe wawili umekamilika baada ya dakika 90 huku pointi tatu zote zikibaki nyumbani.
Ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri umesoma Polisi Tanzania 2-0 Mbeya City. Mabao yote mawili yamefungwa na mshambuliaji wa mabao Anuary Jabir dakika ya 38 na 45+2 kwa mkwaju wa penati.
Ushindi huu unaifanya Polisi Tanzania kufikisha jumla ya pointi10 kibindoni huku Mbeya City ikisaliwa na pointi 10.
Mchezo mwingine mkali wa leo ni Coastal Union vs JKT Tanzania huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Coastal Union ina pointi4 inawakaribisha JKT Tanzania wenye pointi 7 kibindoni.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.