Mashujaa FC vs Singida Black Stars NBC Premier League

Leo Septemba 9, 2026 mchezo mkali wa NBC Premier League unatarajiwa kuchezwa kwa wababe wawili kusaka pointi tatu muhimu Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma.

Mashujaa FC iliyo nafasi ya 10 na pointi 6 baada ya mechi 5 inakutana na Singida Black Stars iliyo nafasi ya 4 na pointi 10 baada ya mechi 5.

Mchezo huu utapigwa saa 10:00 jioni huku timu zote zikibainisha kwamba zipo tayari kwa pambano hilo kali ndani ya uwanja.

Huu ni mchezo wa mzunguko wa 6 kwa timu hizi mbili ambazo zinawania taji la Ligi Kuu Bara lililo mikononi mwa Yanga SC inayoongoza ligi ikiwa na pointi 15 baada ya mechi 5.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Duniani kote kinapatikana mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.