Meridianbet yaonyesha upendo kwa wazee wa Tabata Kisukuru

Kwenye maisha, afya bora ni mtaji mkubwa, lakini wakati mwingine mahitaji madogo ya kila siku yanaweza kuwa changamoto kubwa kwa baadhi ya watu. Hilo ndilo lililomfanya Meridianbet kupeleka moyo wake wa kijamii hadi Tabata Kisukuru, Dar es Salaam, ambapo ilifanya ziara katika The Community Centre for Preventive Medicine na kuwafikishia msaada wazee wanaoishi katika taasisi hiyo.

Meridianbet ilifika ikiwa na msaada wa mahitaji muhimu yaliyolenga kugusa moja kwa moja maisha ya wazee hao. Miongoni mwa vitu vilivyokabidhiwa ni mchele, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni za unga na sabuni za vipande pamoja na vifaa vya usafi binafsi. Mahitaji hayo yana nafasi muhimu katika kuhakikisha kituo kinaendelea kutoa huduma katika mazingira yanayozingatia usafi na upatikanaji wa chakula.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mahusiano wa Meridianbet, Nancy Ingram, alisema kampuni hiyo inatambua mchango ambao wazee wameutoa katika jamii na kuona ni jukumu lake kuwapa msaada na faraja wanapohitaji. Ujumbe huo uliweka wazi dhamira ya Meridianbet ya kuendelea kuwa karibu na jamii na kushiriki katika changamoto zinazoikabili.

Kwa upande mwingine, uongozi wa The Community Centre for Preventive Medicine ulieleza kufurahishwa na hatua ya Meridianbet, wakisema msaada huo umefika wakati muhimu na umesaidia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vyakula na vifaa vya usafi. Taasisi hiyo inaendelea kuwa sehemu muhimu katika kuwahudumia wazee, hivyo ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali una nafasi kubwa katika kuimarisha huduma.

Lakini kilichobeba uzito mkubwa zaidi katika ziara hiyo ni muda ambao wafanyakazi wa Meridianbet walitumia pamoja na wazee. Mazungumzo ya karibu, kucheka na kushirikiana yaliifanya siku hiyo kuwa ya furaha na kuacha kumbukumbu nzuri. Meridianbet imeonyesha kuwa wakati mwingine zawadi kubwa si kitu unachokabidhi, bali ni muda na upendo unaompa mwingine.