Msimu mpya wa Serie A unaanza kwa mlipuko mkubwa mabingwa dhidi ya timu iliyopanda daraja. Mechi hii itachezwa leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, kwenye dimba la San Siro (Giuseppe Meazza), jijini Milan, kuanzia saa 19:30 usiku hii ni mechi ya kwanza kabisa ya Matchday 1 kuchezwa msimu huu, ikiwapa mashabiki fursa ya kuona mabingwa wakianza safari ya kutetea taji lao.
Inter wanaingia mechi hii wakiwa na kila sababu ya kuwa na kujiamini. Msimu uliopita walimaliza kwa pointi 87, wakiibuka mabingwa mechi tatu kabla ya msimu kwisha, na kumaliza msimu mzima wakiwa hawajapoteza mechi nane mfululizo takwimu inayothibitisha uimara wao wa kimfumo chini ya kocha Cristian Chivu.
Tofauti na msimu uliopita ambapo alikuwa bado anajijenga, msimu huu ni wa kwanza ambao Chivu ataanza akiwa kocha mkamilifu wa timu tangu mwanzo hadi mwisho. Kwenye soko la wachezaji, klabu imeongeza nguvu ulinzini kwa kumpata Djed Spence kutoka Tottenham, ikionyesha nia ya kuendelea kuboresha kikosi hata baada ya kutwaa ubingwa.
Kwa upande mwingine, Monza wanarudi Serie A wakiwa na hisia mchanganyiko furaha ya kupanda daraja mara moja baada ya kushuka, lakini pia wasiwasi wa kukutana na mabingwa watetezi mchezo wao wa kwanza kabisa. Ni fursa ngumu kianzia, kwani watalazimika kuonyesha uimara wa haraka dhidi ya timu iliyo bora zaidi nchini Italia kwa sasa.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Michezo ya hivi karibuni kati ya timu hizi mbili inampa Inter faida. Kati ya mechi tano za mwisho, Inter walishinda mara tatu, huku matokeo ya karibuni yakiwemo ushindi wa 2-0 wa Inter nyumbani msimu wa 2023-24, na mfululizo wa mechi mbili msimu wa 2024-25 ambapo walichezea sare 1-1 ugenini kisha kuwashinda tena wakiwa nyumbani. Historia hii inaonyesha kwamba, hasa wanapocheza San Siro, Inter huwa vigumu kuwazuia.
Inter wana kila sababu ya kuanza msimu kwa ushindi. Hata hivyo, mechi za kwanza za msimu mara nyingi huwa na mizani tofauti na inavyotarajiwa Monza watakuwa na kila motisha ya kuonyesha ujasiri wao mbele ya mashabiki wa mabingwa.