Mchezo umekamilika kwa wababe wawili katika msako wa pointi 3 muhimu ubao wa Uwanja wa Airtel umesoma Singida Black Stars 1-2 Simba SC.
Wenyeji Singida Black Stars wamepata bao kupitia kwa nyota Shekhan Ibrahim ilikuwa dakika ya 23.
Kwa upande wa Simba SC ambao walikuwa ugenini wamepata mabao kupitia kwa kiungo mshambuliaji Clatous Chama dakika ya 11 na beki De Reuck dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati mara baada ya Traore kuchezewa faulo ndani ya 18.
Mchezo wa 3, Simba SC mchezaji watatu anaonyeshwa kadi nyekundu ambaye ni beki Anthony Mligo ilikuwa dakika ya 84.
Mchezo wa kwanza alionyeshwa Duchu dhidi ya Kagera Sugar na mchezo wa pili ni Ibraheem dhidi ya Pamba Jiji FC.
Simba SC inafikisha pointi 9 baada yakucheza mechi 3 imepata ushindi mechi zake zote mpaka sasa ikiruhusu mabao mawili yakufungwa na imefunga mabao 6.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.