Klabu ya Paris Saint-Germain imepata habari njema kuelekea fainali ya UEFA Champions League baada ya nyota wao Ousmane Dembele na Achraf Hakimi kurejea mazoezini kikosini.
Dembele alikuwa nje baada ya kupata majeraha ya misuli ya mguu wa kulia katika mchezo wa Ligue 1 dhidi ya Paris FC uliochezwa Mei 17, 2026.
Kwa upande wa Hakimi, beki huyo alipata majeraha ya paja la kulia katika ushindi wa kusisimua wa nusu fainali dhidi ya Bayern Munich, lakini sasa ameonekana kurejea katika mazoezi kamili ya timu hiyo.
PSG ambao ni mabingwa watetezi wanatarajiwa kuvaana na Arsenal F.C. katika mchezo wa fainali ya Champions League utakaopigwa jijini Budapest siku ya Jumamosi.