KMC FC ni sikio la kufua kutokana na kuwa na rekodi isiyofurahisha kwa msimu wa 2025/26 kutokana na matokeo kutokuwa mazuri ndani ya ligi huku ikiwa ni kinara kwenye kufungwa magoli mengi ndani ya ligi.
Timu hiyo inayotumia Uwanja wa KMC Complex baada ya mechi 25 imekusanya jumla ya pointi 9 ikiwa imepata ushindi kwenye mechi 2 pekee.
Imefungwa jumla ya magoli 43 ikiwa ni timu namba moja kwa kuruhusu magoli mengi na safu ya ushambuliaji imefunga magoli 13. Ipo kwenye mstari wa kushuka daraja ikiwa nafasi ya 16 kwenye msimamo.
Timu ambayo imefunga magoli mengi ni Yanga SC ikiwa nayo 58 baada ya mechi 25 inafuatiwa na Simba SC iliyofunga magoli 45 katika ligi namba 6 kwa ubora.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.
Soccer Football - International Friendly - Spain v Brazil - Santiago Bernabeu, Madrid, Spain - March 26, 2024 Spain's Rodri scores their third goal from the penalty spot REUTERS/Violeta Santos Moura