Mashabiki wa soka duniani wamebaki MIDOMO WAZI baada ya dabi kali ya Riyadh kati ya Al-Nassr FC na Al-Hilal SFC kumalizika kwa sare ya 1-1 kwenye uwanja wa Al-Awwal Park!
Kila kitu kilionekana kwenda upande wa Cristiano Ronaldo baada ya Mohamed Simakan kufunga bao safi dakika ya 37 kupitia krosi ya Kingsley Coman. Mashabiki wa Al-Nassr walikuwa tayari wanaanza sherehe za ubingwa!
LAKINI SOKA HALINA HURUMA!
Dakika ya 90+8, mpira wa kutupwa ndani uliletwa moja kwa moja eneo la hatari, kipa Bento Krepski akashindwa kuudhibiti na kujifunga mwenyewe!
Bao hilo limeahirisha sherehe za ubingwa za Al-Nassr na kuifanya vita ya taji la Saudi Pro League kuwa moto zaidi huku zikiwa zimebaki mechi chache kumaliza msimu.