Dodoma Jiji FC vs Yanga SC, Zimbwe Jr anafuatiliwa

Dodoma Jiji FC vs Yanga SC ni leo Mei 13, 2026 NBC Premier League Uwanja wa Airtel saa 10:15 jioni.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Yanga SC, Ahamid Moallin amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo isipokuwa Zimbwe Jr anafuatiliwa kwa ukaribu maendeleo yake.

“Wachezaji wote wako salama na tayari kwa mchezo isipokuwa tunamfuatilia Mohammed Hussein ambaye ameanza kurejea mazoezini baada ya kuumia. Tutategemea tathmini ya mwisho kutoka kwa madaktari kuona kama atakuwa tayari kucheza. Pia ni jambo zuri kuwa Mudathir aliyekuwa kwenye adhabu ya kusimamishwa kurejea kikosini.

“Kila mchezo kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu ni muhimu sana kwetu. Benchi la ufundi, wachezaji pamoja na uongozi wote tunafanya kazi kuhakikisha tunapata pointi tatu katika kila mchezo,”.

Yanga SC ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ina pointi 54 inakutana na Dodoma Jiji FC iliyo nafasi ya 8 na pointi 29.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.