Simba SC vs Tanzania Prisons kupigwa KMC Complex saa 1:00 jioni ukiwa ni mchezo wa NBC Premier League.
Tayari viingilio vimetajwa ambapo mzunguko ni 10,000 na VIP 20,000 kushuhudia burudani ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba 6 kwa ubora.
Kwenye msimamo Simba SC ni nafasi ya pili ikiwa na pointi 46 inakutana na Tanzania Prisons ambayo ipo nafasi ya 15 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 14.
Prisons inapambana kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja inakutana na Simba SC ambayo inapambana kusaka pointi tatu kuendeleza matumaini ya vita ya ubingwa wa ligi.
Mchezo uliopita Simba SC ilipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya JKT Tanzania ulichezwa Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo ambao ulikuwa unatumika kwa mechi za nyumbani kabla hawajatangaza kuhamia Uwanja wa KMC Complex, Dar.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.