Simba SC vs Yanga SC kiingilio hiki hapa Kariakoo Dabi

Simba SC vs Yanga SC ni mchezo unaofuata kwenye ratiba ya NBC Premier League kwa wababe hawa wawili kusaka pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.

Vinara ni Yanga SC wakiwa na pointi 47 huku Simba SC ikiwa nafasi ya pili na pointi 42 tofauti ya pointi 5 kwa wababe hawa wawili.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex ulisoma Yanga SC 0-0 Simba SC wakigawana pointi mojamoja.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo huo kutokana na umuhimu na amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu kutokana na umuhimu wa pointi tatu hautakuwa mchezo mwepesi hasa ukizingatia tumetoka kupata ushindi mchezo uliopita fainali ya Muungano.

“Hatujataka kuweka viingilio vya kausha damu ili kila Mwanasimba aweze kuingia, kwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo tungeweka viingilio vikubwa. Lakini tumeweka viingilio rafiki. Mkanunue tiketi mapema,” amesema Ahmed.

Miongoni mwa wachezaji wa Simba SC waliopo kwenye maandalizi kuelekea mchezo huo ni Ellie Mpanzu, Clatous Chama, Hussen Abel na Seleman Mwalimu.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.