Simba SC amechukua alama zote tatu ugenini dhidi ya Wauaji wa Kusini, Namungo FC katika dimba la Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu bara.
Mnyama amesogea mpaka alama tano nyuma ya vinara Wananchi, Young Africans SC wakifikisha alama 42 baada ya mechi 19 wakiwa nafasi ya pili huku Namungo FC wakisalia nafasi ya 10 alama 22 baada ya mechi 19.
FT: Namungo FC 1-3 Simba SC
⚽ 33’ Makambo (P)
⚽ 12’ Libasse Gueye
⚽ 25’ Anicet Oura
⚽ 74’ Ellie Mpanzu