JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa maandalizi yamekamilika na vijana wapo tayari kwa mchezo wa leo vs Simba SC.
Namungo FC vs Simba SC ni mchezo wa NBC Premier League unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa huku wageni wakiwa ni Simba SC.
Hii ni ligi namba 6 kwa ubora ushindani unekuwa mkubwa kutokana na kila timu kupambana ndani ya uwanja kusaka pointi tatu muhimu.
Mgunda amesema:”Maandalizi yapo tayari kuelelea mchezo wetu dhidi ya Simba SC, tunatambua utakuwa mchezo wenye ushindani tukiwa nyumbani, mashabiki wajitokeze kwa ajili ya kutushangalia,”.
Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema anatambua mchezo utakuwa na ushindani wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
“Tumefanya maandalizi mazuri tunatambua utakuwa ni mchezo mgumu. Tunahitaji kucheza vizuri na kupata matokeo mazuri,”.
Simba SC kwenye msimamo nafasi ya 2 inakaribishwa na Namungo FC iliyo nafasi ya 10.
Mshambuliaji namba moja kwa anamungo FC ni Fabrice Ngoyi amefunga magoli 8 kwa upande wa Simba SC yupo Seleman Mwalimu mwenye magoli 6.