Singida Black Stars 5-1 Mbeya City FC matokeo ya mchezo wa leo Aprili 12, 2026 kwenye hatua ya 16 bora CRDB Federation Cup.
Ni mchezo ambao umechezwa Uwanja wa Airtel huku wenyeji Singida Black Stars wakikata tiketi yakutinga hatua ya robo fainali kwa ushindi mnono dhidi ya wageni ndani ya dakika 90.
Magoli ya Singida Black Stars yamefungwa na Khalid Aucho dakika ya 16, Lamine Jarjou dakika ya 58, Ibrahim Imoro alitupia mawili dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 78 na kamba ya 5 ilifungwa na Horso Mwaku dakika ya 66.
Ni Daniel William alipachika goli pekee kwa Mbeya City kwenye mchezo wa leo dakika ya 81 likiwa ni goli la kufutia machozi.
Matokeo hayo yanawafugashia virago Mbeya City huku Singida Black Stars wakitinga hatua ya robo fainali.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.
Curacao's players pose for a team photo before the start of the World Cup qualifier football match between Jamaica and Curacao at the National Stadium in Kingston, Jamaica on November 18, 2025. (Photo by Ricardo Makyn / AFP) (Photo by RICARDO MAKYN/AFP via Getty Images)