
Leo tarehe 12 Aprili saa 16:00, Uwanja wa Stadium of Light utakuwa mwenyeji wa pambano la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kati ya Sunderland na Tottenham Hotspur.
Mechi hii ina umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili lakini kwa sababu tofauti kabisa. Tottenham wako katika mzumu wa kushuka daraja, wakiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo na pointi 30 pekee baada ya mechi 31, huku wakiwa na rekodi mbaya ya mechi 5 mfululizo bila ushindi.
Kwa upande mwingine, Sunderland wana ndoto za kufuzu Uropa, wakiwa nafasi ya 4 kwenye msimamo na wamekuwa wakiongeza kasi, ikiwemo ushindi wa kimtindo katika derby ya mitaa dhidi ya Newcastle . Mwamuzi Robert Jones ndiye atakayesimamia mechi hii.
Tottenham wataingia uwanjani wakiwa na kocha mpya, Roberto De Zerbi, ambaye anachukua mikoba baada ya kuachana na Igor Tudor. Hii ni mechi yake ya kwanza akiongoza Spurs, na anatarajiwa kuleta falsafa yake ya umiliki wa mpira na mashambulizi makali .
Kwa upande wa majeruhi, Tottenham wanakabiriwa na wachezaji watano wanaorejea Rodrigo Bentancur, Ben Davies, Mohammed Kudus, Pape Matar Sarr na Mathys Tel wako karibu kucheza. Hata hivyo, James Maddison, Dejan Kulusevski na golikipa Vicario bado wako nje. Sunderland wana majeruhi wawili muhimu (Nilson Angulo, Bertrand Traore), lakini wana habari njema kwa kurejea kwa beki Dan Ballard .
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Hata hivyo, msimu huu Sunderland wamekuwa hodari nyumbani (Stadium of Light), wakiwa na rekodi nzuri ya kushinda timu kubwa, hivyo wataingia uwanjani wakiwa na imani kubwa.
Kwa Sunderland, Kocha Regis Le Bris ana timu yenye nidhamu ya ulinzi na wanaweza kukaa nyuma kisha kushambulia kwa kasi . Wachezaji kama Chemsdine Talbi na Brian Brobbey wamekuwa wakiwapa nguvu ya ushambuliaji .
Kwa upande wa Tottenham, De Zerbi atalazimika kurekebisha safu ya ulinzi iliyokuwa ikivuja mabao mengi wamekosa ushindi wa Ligi tangu Desemba. Timu hii bado ina wachezaji hatari kama Richarlison (mabao 9 msimu huu) na wao ni hatari sana kwenye mpira wa kona .
Mechi ya leo ni fursa kwa De Zerbi kuanza vizuri ukocha wake Tottenham, lakini anaikuta Sunderland iliyojaa kujiamini na wachezaji wao muhimu wakiwa wamerudi. Tottenham wanahitaji pointi kukimbia eneo la kushuka daraja (wako pointi 1 tu juu ya West Ham), lakini kiwango chao cha sasa hakitoi tumaini kubwa. Jisajili