Simba SC 3-1 Dodoma Jiji FC, CRDB Federation Cup

Simba SC 3-1 Dodoma Jiji FC, CRDB Federation Cup ni matokeo rasmi kwenye mchezo wa leo hatua ya 16 bora mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Simba SC wenyeji waliruhusu goli la mapema dakika ya 9 ambalo lilidumu mpaka muda wa mapumziko ubao ulipokuwa ukisoma Simba SC 0-1 Dodoma Jiji FC.

Nyota wa Dodoma Jiji FC Khleffin Hamdoun alianza kupachika goli la uongozi dakika ya 9 ambalo hilo lilidumu mpaka dakika ya 53 ya mchezo.

Magoli ya Simba SC yamefungwa na Seleman Mwalim aliyepachika mawili dakika ya 54 na 67 huku goli moja likifungwa na Anicet Oura dakika ya 60.

Nyota wa mchezo amechaguliwa kuwa Seleman Mwalimu akipewa zawadi ya laki 5 na wadhamini CRDB  huku mnyama akitinga hatua ya robo fainali.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.